Vipengee vya Chapa

Mwongozo wa nembo

Nembo yetu ni ishara muhimu zaidi inayowakilisha ProBit Global na ina jukumu muhimu katika kutoa dhana ya chapa yake. Kwa hivyo, umbo na uwiano wa vipengee vyote kwenye nembo lazima ubaki jinsi ulivyo. Inapendekezwa kutumia muundo wima. Ni wakati tu ambapo haiwezekani, ndipo muundo mlalo unaweza kutumika.

Wima
Mlalo

Mwongozo wa jina la chapa

Unapoandika jina la chapa ya ProBit Global, yafuatayo yanapaswa kufuatwa ili kupunguza hali ya kuchanganyikiwa.

Kila herufi ya jina la chapa yetu inaweza kuandikwa kwa herufi kubwa.

Herufi ‘B’ ya neno ‘ProBit’ inapaswa kuwa herufi kubwa.

Neno ‘ProBit’ halipaswi kutumika peke yake.

Nafasi inapaswa kuwekwa kati ya neno ‘ProBit’ na ‘Global’ ili kuyatofautisha.

Mwongozo wa rangi

ProBit Global Ultramarine ni rangi ya chapa inayoashiria ProBit Global. Unaweza kuchagua kati ya rangi zilizo kwenye kibao kifuatacho cha kuchanganyia rangi nzito ya bluu inayong'aa ili itoe mwangaza bora wa mandharinyuma meupe au meusi.

PROBIT GLOBAL Ultramarine

HEX #4231c8
RGB 66 49 200
CMYK 90 90 0 0
PANTONE 2369 C

Ultramarine (For Dark Theme)

HEX #504ced
RGB 80 76 237
CMYK 83 71 0 0

PROBIT GLOBAL Gray

HEX #7b7b7b
RGB 123 123 123
CMYK 60 52 48 0

Mwongozo wa ushirikiano

Wakati nembo ya ProBit Global inaonyeshwa pamoja na nembo ya mshirika, tafadhali rejelea picha hii na usibadilishe nafasi na ukubwa wa nembo. Ikiwa ni lazima ufanye mabadiliko, hakikisha uwiano wake unadumishwa na panapaswa kuwa na nafasi dhahiri ya kutosha karibu na nembo.

Vizuizi

Umbo na uwiano wa nembo yetu lazima udumishwe na mabadiliko yoyote yasiyo na msingi maalum hayaruhusiwi ikijumuisha urekebishaji na mabadiliko ya kipengele, athari au rangi.

Usipanue au kuinamisha mwonekano na ukubwa wa nembo.

Usiongeze au kuwekelea juu mandharinyuma nyuma ya nembo.

Usibadilishe umbo au nafasi ya vipengele vya nembo.

Usitumie mchanganyiko wa rangi usio na msingi maalum.

Usibadilishe fonti za nembo.

Usiweke athari ya kivuli kwenye nembo.

Usiweke mpaka kwenye nembo.

Usitumie toleo la zamani la nembo.

Usibadilishe rangi ya nembo.

Usibadilishe muundo wa nembo.